IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tunisia mwaka huu hayafanyiki kutokana na ukosefu wa bajeti

11:03 - May 23, 2016
Habari ID: 3470328
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tunisia mwaka huu hayatafanyika kutokana na ukosefu wa bajeti.

Wizara ya Masuala ya Kidini Tunisia imesema bajeti iliyokuwa itumike kwa ajili ya mashindano hayo imetengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo wa watu 100,000 wanaopewa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani nchini humo.

Amesema mpango huo unahitaji bajeti kubwa na kwa kzungatia bajeti ndogo iliyotengewa shughuli za Qur'ani nchini humo, mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tunisia hayatafanyika kama ilivyokuwa imepangwa.

Mpango huo wa kutoa mafunzo kwa wenye kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Tunisia ulianza mwezi Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa mpango huo, Watunisia laki moja watafunzwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tunisia hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis kwa kuwashirikisha makumi ya quraa na hufadh wa Qur'ani kutoka maeneo yote duniani.

3459897

captcha