Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Al Furqan' yanafanyika kwa himaya ya Jumuiya ya Sayansi za Qur'ani ya Iqraa.
Mashindano hayo yaliyopanga kuanza tarehe mosi Julai yanafanyika pia kwa ushirikiano na Jumuiya ya Ahul Bayt AS ya Kuwait na yatakuwa na vitengo vya wanawake na wanaume.
Imearifikuwa kuwa mashindano hayo yatakuwa na makundi mawili ya umri wa vijana wa miaka 15 kuendelea ambao watashindano kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na pia tafsiri ya Surat Mursalat.
Aidha kutakuwa na kundi la walio na umri wa miaka 15 watakashindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na tafsiri ya Surat Naml.
Jumuiya ya Sayansi za Qur'ani ya IQRA metangaza kuwa tarehe 10 Juni ni siku ya mwisho ya kuwasajili washiriki wa mashindano hayo ya Qur'ani.