IQNA

Kuanzia Kuhifadhi Qur'ani utotoni hadi kuisoma ndani ya Kaaba: Safari ya Qur'ani ya Sheikh Tablawi

13:38 - June 14, 2016
Habari ID: 3470384
IQNA-Sheikh Muhammad Mahmoud Tablawi, mmoja wa maqari mashuhuri na wenye taswira ya kipekee nchini Misri, alifariki dunia miaka sita iliyopita baada ya kutumikia Qur'ani Tukufu kwa zaidi ya miaka sitini.

Sheikh Tablawi, ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasomaji Qurani na Waliohifadhi Qur’ani Misri aliaga dunia baada ya kuihudumia Qur’ani kwa muda wa miaka 60.

Msemaji wa Jumuiya ya Wasomaji Qurani na Waliohifadhi Qur’ani Misri ametuma risala za rambi rambi kwa niaba ya wanachama wenzake.

Nayo Dar ul Iftaa ya Misri imetuma salamu za rambi rambi kufuatia kauga dunia qarii huyo mashuhuri wa Qur’ani Tukufu.

Mohamed Mahmoud Tablawi alizaliwa Novemba 14, 1934 katika kijiji cha Met Oqna nchini Misri. Alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri wa miaka mine na kuhitimua akiwa na umri wa miaka 9. Alipata taufiki ya kusafiri katika nchi nyingi duniani akiwa mwakili wa Al-Azhar na Wizara ya Wakfu ya Misri. Halikadhalika aliwahi kuwa jaji katika mashindano mengi ya Qur’ani ya kimataifa.

 

Kishikizo: tablawi
captcha