IQNA

Tahadhari kuhusu kusambazwa Qur'ani zenye makosa ya chapa nchini Sudan

16:40 - July 12, 2016
Habari ID: 3470450
Sheikh Mohammad Hashim Al Hakim, mwanachama wa Jumuiya ya Maulamaa wa Sudan ametahadharisha kuhusu kusambazwa nakala za Qur'ani nchini humo ambazo zina makosa ya chapa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya alnilin imeandika kuwa,Sheikh Mohammad Hashim al Hakim, mwanachama wa Jumuiya ya Maulamaa wa Sudan ambaye pia ni mwanachama wa Baraza Kuu la Maulamaa Waafrika ambaye amesema: "Kuna nakala za Qur'ani zenye makosa ya chapa ambazo zimesambazwa kote Sudan."

Ameongeza kuwa, nakala hizo za Qur'ani zimechapishwa na taasisi moja ya Syria na Misri na ambaye ilipata idhini nambari 26 ya uchapishaji Februari mwaka 2015 kutoka kwa Idara ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar.

Al Hakim amesema aya 64 za Sura Aal Imran zimefutwa katika ukurasa wa 10 wa nakala hizo za Qur'ani.

Mwanachuoni huyo wa Sudan amehoji ni vipi nakala hizo za Qur'ani zimeingia nchini humo.

Ametaka Wizara ya Awqaf, Idara ya Forodha na taasisi zingine husika kuzingatia na kuchunguza zaidi kadhia hii.

3514455

captcha