Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanaofika katika katika meza hiyo hupata Qur'ani Tukufu iliyofasiriwa kwa Kiingereza au Kihispania mbali na vitabu kuhusu Maisha na Sirah ya Mtume SAW. Halikadhalika kuna kitabu kuhusu masuala 50 ambayo watu huuliza mara kwa mara kuhusu Uislamu.
Dkt. Sabeel Ahmed, Mkurugenzi wa GainPeace anasema, "Kuna matumaini kuwa, kwa kusoma Uislamu kutoka chanzo chake asili yaani Qur'ani Tukufu, wasomi wanaweza kufahamu kuwa Uislamu unaping autumiaji mabavu, mauaji, dhulma na dini hii inatetea uadilifu na ulindwaji maisha ya wote."
Amesema mwaka huu pekee, GainPeace imekuwa na vibana 105 Chicago na pia miji ya Detroit na Kansas Marekani na pia Toronto nchini Canada.
GainPeace ni mradi wa Mtandao wa Kiislamu Amerika ya Kaskazini na ni kati ya taasisi kubwa za Waislamu katika eneo hilo.