IQNA

Pakistan yazindua hadithi za Qur’ani kwa watoto

21:02 - August 02, 2016
Habari ID: 3470489
Taasisi ya Kitaifa ya Vitabu Pakistan imezindua kitabu maalumu cha hadithi za Qur’ani maalumu kwa watoto wadogo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kitabu hicho kilichopewa jina la ‘Qur’an Khani (kusoma Qur’ani) kimeandikwa na Dkt. Qadri Muhammad Tahir.

Imearifiwa kuwa kitabu hicho kimetayarishwa kwa mbinu maalumu yenye uwezo wa kulea watoto wenye maadili mema, afya ya kiakili na elimu bora. Aidha kitabu hicho kinalenga kulea kizazi cha watoto wenye uwezo wa kuwa na nafasi nzuri na yenye manufaa katika jamii.

Kitabu cha Qur’an Khani kimeandikwa kwa mujibu wa hadithi tisa muhimu za Qur’ani ili kwa njia hiyo kufikisha ujumbe wenye mafunzo kwa watoto.

3460575

Kishikizo: watoto qurani iqna pakistan
captcha