IQNA

Mtoto wa miaka mitatu ahifadhi Qur’ani kikamilifu nchini Nigeria

0:14 - August 08, 2016
Habari ID: 3470503
Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu amefanikiwa kuhifadhi kikamilifu Qur’ani Tukufu katika mji wa Zaria kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wazazi wa Muhammad Shamseddin Ali walimpeleka katika Chuo cha Kimataifa cha Kuhifadhi Qur’ani cha Sheikh Anju Abdullah akiwa na umri wa miaka 1.5

Shule hiyo ni maalumu kwa ajili ya kutoa manfuzo ya Qur’ani kwa watoto wadogo.

Baba yake Muhammad, Sheikh Shamseddin Ali, ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho, amesema sababu ya kuwasomesha watoto wadogo kuhifadhi Qur’ani ni kuwa ubongo huweza kuhifadhi mengi kirahisi katika umri huo.

Akizungumza kuhusu mafanikio ya mwanae anasema: "Tunaamini kuwa wakati mtoto anapoachishwa maziwa ya mama, (akiwa na umri wa miaka miwili) hadi wakati wa kubaleghe, ubongo huwa wazi na hivyo kumuwezesha mtoto kuhifadhi kirahisi anayofunzwa. Hii ndio sababu tunawachukua watoto kuanzia umri huo, haswa kwa ajili ya kuhifadhi Qur’ani.”

Anaendelea kusema kuwa: "Muhammad si mtoto pekee mwenye uwezo wa kuhifadhi Qur’ani Tukufu hapa, lakini tafauti yake na wengine ni kuwa, ameweza kushinda mashindano kadhaa ya kimataifa. Hapa tuna watoto kutoka kote Nigeria ambao wanasoma Qur’ani Tukufu na pia masomo yote ya watoto wa chekechea ikiwa ni pamoja na lugha za Kiarabu na Kiingereza.”

Sheikh Shamseddin Ali amebaini kuwa awali mke wake hakuridhia kumpelekea mtoto mdogo sana chuoni lakini alitulia alioona alivyoanza kunawiri katika kuhifadhi Qur’ani.

Mji wa Zaria umepata umashuhuri kimataifa kutokana na kuwa makao ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky.


3520690

captcha