Duru zinaarifu , wafanyakazi wa kituo hicho kwa muda wa miezi kadhaa sasa wametoa wito kwa wahusika kulipa mishahara kwa wakati. Hatahivyo wakuu wa kituo hicho wamepuuza takwa la kulipa mishahara kwa wakati na hivyo kuwalazimu wafanyakazi kuandamana.
Wafanyakazi wa Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd wanasema kuwa kutokana na kucheleweshwa mishahara yao wamekumbwa na matatizo ya kifamilia.
Nakisi kubwa na isiyo na kifani ya bajeti ya Saudi Arabia kutokana na uingiliaji kijeshi ufalme huo katia nchi jirani ya Yemen na pia kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi za eneo ni mambo ambayo yamepelekea watawala wa ukoo wa Aal Saud kujipata katika hali ngumu.
Mwezi Aprili , baada ya kuchapishwa ripoti ya Mfuko wa Uwekezaji Saudia kuhusu nakisi ya bajeti ya makumi ya mabilioni ya dola, Mfuko wa Kimataifa wa Fedha IMF ulitangaza kuwa Saudia inakumbwa na nakisi ya dola bilioni 140 katika bajeti yake na kuongeza kuwa, nchi hiyo haina budi ila kutafuta njia za kukabiliana na tatizo hilo.
Pamoja na kuwa kwa muda mrefu Saudia imekuwa na pato kubwa la mafuta
lakini haijaweza kuwawekea wananchi wake suhula bora za maisha na kwamba
takribani asilimia 70 ya raia wa nchi hiyo wana maisha mabovu na hali
mbaya ya kiuchumi.