Akizungumza hapo Jumamosi kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 10 wa ushindi
wa Hizbullah katika vita vya siku 33 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa
Israel, Sayyid Hassan Nasrallah amesema makundi ya kigaidi kama Daesh
yanapaswa kuzinduka na kutambua yanapigana kwa niaba ya nani.Trump majuzi alisema kuwa kundi la ISIS/Daesh lilibuniwa na Rais Barack Obama wa Marekani kwa ushirikiano wa karibu na Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye kwa sasa anagombea kiti cha urais kwa tiketi ya Democrats.
Tarehe 12 Julai mwaka 2006 jeshi la Israel lilishambulia ardhi ya
Lebanon kwa muda wa siku 33 na halikufanikiwa kufikia hata lengo moja
katika mashambulizi hayo kutokana na mapambano ya kishujaa ya
wanamuqawama wa Hizbullah. Wananchi 1,200 wa Lebanon aghalabu yao wakiwa
raia wa kawaida waliuawa huku Wazayuni 160 akthari yao wakiwa ni askari
vamizi wa utawala ghasibu wa Israel wakiangamizwa katika vita hivyo.