Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina, jana zilitoa taarifa za kupinga kuhudhuria Abbas mazishi ya Peres ziliyemtaja kuwa chinjachinja wa Qana.
Katika taarifa yake, Hamas imesema hatua hiyo ya Abbas itafungua njia kwa watu na makundi mengine haini na saliti yanayotafuta fursa ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni.
Kwa upande wake, Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina imetangaza kupitia taarifa yake kuwa kushiriki Mahmoud Abbas na kiongozi mwengine yeyote wa Kipalestina katika mazishi hayo kutatoa pigo kubwa mno kwa wananchi wa Palestina.
Katika salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Peres, Abbas alieleza kusikitishwa na kifo chake na kumtaja kiongozi huyo muuaji wa Kizayuni kuwa ni mtetezi wa amani.
Salamu hizo za rambirambi za Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina zimekabiliwa na radiamali kali za upinzani ndani ya Palestina huku maelfu ya Wapalestina wakizitaja kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni "salamu za mkono wa pole kwa mnywa damu"
Shimon Peres, rais wa zamani wa utawala haramu wa Israel amehusika na jinai nyingi za kinyama dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina ikiwemo kukandamiza Intifadha ya Wapalestina, kusababisha maelfu ya Waplestina kupoteza makaazi yao na kuwa wakimbizi pamoja na mauaji ya Qana.../