IQNA

Maimamu wa Misikiti katika nchi zenye Waislamu wachache kukutana Misri

18:09 - October 02, 2016
Habari ID: 3470592
Mkutano wa kimataifa wa Maimamu wa Misikiti katika nchi zenye Waislamu wachache umepangwa kufanyika, Cairo mji mkuu wa Misri.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mkutano huo utafanyika chini ya kaulimbiu ya 'Mafunzo ya Kuwawezesha Maimamu wa Misikiti katika Nchi Zenye Waislamu Wachache' na umeandaliwa na Idara ya Darul Ifta ya Misri kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Fatwa. Mkutano huo utakuwa na washiriki kutoka zaidi ya nchi 80 duniani na utafanyika kuanzia Oktoba 17-18.

Sheikh Shouqi Alam , Mufti Mkuu wa Misri ambaye pia ni katibu mkuu wa mkutano huo amesema: "Maimamu wa Misikiti na wahubiri wa Kiislamu katika nchi za Magharibi wana jukumu muhimu katika kueneza Uislamu sahihi duniani. Lengo la mkutano huu ni kuwafahamisha Maimamu na wahubiri wa Kiislamu katika nchi za Magharibi kuhusu ufahamu wa sheria za Kiisalmu, maingiliano katika jamii na uhakika wa mambo katika jamii." Amesema kikao hicho pia kitatoa mafunzo kuhusu mbinu sahihi za kufanya mazungumzo ya kidini sambamna na kueneza misimamo ya wastani na kujiweka mbali na misimamo mikali na ya kufurutu adha.

Sheikh Shouqi Alam  ameongeza kuwa,  kikao hicho pia kitachungumza masuala muhimu yanayhusiana na Waislamu waliowachache katika nchi za Magharibi na namna Maimamu wa misikiti wanavyoweza kutatua na kutafutia ufumbuzi tatizo la misimamo mikali ya kidini miongoni mwa jamii za Waislamu waliowachache.

Mkutano huo wa Cairo pia utajadili pia njia za kuimarisha uhusiao baina ya wahubiri, Maimamu wa Misiki na vyuo vikubwa cya Kiislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu. Halikadhalika washiriki watapewa mafunzo kuhusu Fatwa na namna ya kukabiliana na changamoto katika jamii za Waislamu wachache katika nchi za Magharibi na kwingineko duniani.

3534298

captcha