IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Chuo Kikuu cha Theolojia ya Kiislamu (Hauza) kinahitaji mpango wa mabadiliko

18:46 - October 02, 2016
Habari ID: 3470594
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Hauza au Hawza (Chuo Kikuu cha Theolojia ya Kiislamu) inahitaji kuwa na mpango wa mabadiliko na marekebisho na kulitaja hitajio hilo kuwa muhimu katika mazingira ya sasa.

Ayatullah Seyyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Jumapili alipokutana na wanachama wa Baraza Kuu la Hauza  na kuongeza kuwa Hauza haiwezi kutenganishika na Utawala wa Kiislamu.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, utawala wa Kiislamu unaihitajia Hauza  na kuongeza kuwa,  Hauza inayohitajika na serikali ya Kiislamu inapaswa kuwa na watu wenye uwezo mkubwa wa kifikra, wenye elimu pana, wabunifu na wanaofahamu mahitajio ya dunia ya leo ili waweze kuielemisha jamii kuhusu mafundisho ya Kiislamu katika sekta mbali mbali za maisha. Kiongozi Muadhamu amesema Hauza inapaswa kuwa na mpango wa mabadiliko na pia mpango wa muda mrefu ambao unaweza kutekelezeka, wa kina na wenye muda maalumu ili mabadiliko yafanyike katika fremu hiyo.

Kiongozi Muadhamu amesema Hauza inapaswa kuwa na mipango katika sekta mbali mbali hasa kuhusu wanaohitimu, utekelezwaji na pia kuweza kuenda sambamba na Utawala wa Kiislamu. Amesema Hauza iko mstari wa mbele katika utekelezwaji wa sheria za Kiislamu na kwa msingi huo, iwapo utawala utatekeelza ipasavyo sheria za Kiislamu, Hauza inapaswa kuunga mkono hatua hizo kikamilifu na iwapo utawala utakosea basi Hauza inapaswa kutoa tahadhari. Aidha Ayatullah Khamenei amesema Hauza inapaswa kuwa na 'Kituo cha Utafiti wa Kistratijia' ambacho kitawaleta pamoja wasomi na wanachuo mahiri wa Hauza ili waweze kutayarisha mpango wa mabadiliko na mipango mingine ya kimkakati.

3534799

captcha