IQNA

Saudia yakaidi walimwengu na kukataa uchunguzi wa jinai zake nchini Yemen

9:51 - October 06, 2016
Habari ID: 3470601
Saudi Arabia imeendelea kukaidi wito wa kuundwa kamati ya kimataifa ya kutafuta ukweli kuhusu jinai zilizofanywa na utawala huo dhidi ya taifa la Yemen.

Adel Bin Zayd al-Tarifi, Waziri wa Utamaduni na Vyombo vya Habari wa Saudi Arabia amesema Riyadh haiko tayari kutekeleza wito wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein anayetaka kuundwa tume huru ya kimataifa ya kufanya uchunguzi kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na Saudia nchini Yemen.

Akizungumza jana Jumatano, al-Tafiri alisema Saudia haikubaliani na takwa hilo kwa kuwa tayari Riyadh ilikubali uchunguzi unaofanywa na Kamisheni ya Taifa ya Yemen, ambayo inaripoti moja kwa moja kwa Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais mtoro na aliyejiuzulu wa Yemen.


Kwingineko, hujuma za ndege za kivita za Saudi Arabia na waitifake wake Yemen, mbali na kuwaua maelefu ya raia wa nchi hiyo na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola kwa miundo mbinu ya nchi hiyo, pia zimesababisha zaidi ya watoto milioni mbili Wayemen kukosa masomo.

Katika ripoti yake mpya kuhusu  Yemen, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Watoto UNICEF imetangaza kuwa, kushadidi mapigano kumepelekea kufungwa na kuharibiwa idadi kubwa ya shule katika kipindi cha mwaka moja na nusu ni jambo ambalo limepelekea karibu watoto milioni mbili Wayemen kushindwa kuendelea na masomo huku baadhi ya watoto wakikabiliwa na hatari ya kutumwa katika medani ya vita.

Ripoti ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF inaeleza kuwa, zaidi ya shule elfu mbili na mia moja zimeharibiwa na mashambulio ya Saudia nchini Yemen.

Wasiwasi wa UNICEF kuhusu watoto wa Yemen kukosa kuenda shule kutokana na vita katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo kunajiri wakati ambao idara ya Umoja wa Mataifa nchini Yemen wiki iliyopita ilitoa taarifa kwa munasaba wa kufunguliwa shule na kutoa wito kwa pande hasimu kujizuia kulenga shule vitani. Taarifa hiyo ilisema katika miezi 18 ya vita nchini Yemen, kumejiri uharibifu mkubwa wa miundomsingi ya vituo vya elimu huku idadi kubwa ya wanafunzi na waalimu wakiuawa au kujeruhiwa vitani.

Tangu ulipoanzisha uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka uliopita, hadi sasa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud na kuungwa mkono na Marekani na Israe umesha zishambulia skuli, hospitali, makaazi ya raia,misikiti,  barabara, masoko na kambi za wakimbizi na kuua maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Zaidi ya watu 10,000 wamepoteza maisha katika hujuma ya kinyama ya Saudia dhidi ya Yemen.

Lengo kuu la hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen ni kumrejesha madarakani kibaraka wake, Rais mtoro na  aliyejiuzulu wa nchi hiyo Abd Rabu Mansour Hadi na kuwaondoa madarakani wanamapinduzi wa Ansarullah.

3535928

Kishikizo: yemen saudia jinai vita iqna
captcha