IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Waislamu watapata ufanisi kwa kuwa waangalifu na kudumisha umoja

20:40 - October 28, 2016
Habari ID: 3470638
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameyataka mataifa ya Kiislamu kushikamana na kusimama kidete mbele ya maadui wa Uislamu.

Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliouhudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, Waislamu wakiwa na lengo la kuyapatia ufumbuzi matatizo na migogoro ya sasa wanapaswa kuwa macho kikamilifu na wadumishe umoja na mshikamano mbele ya watu ambao katika fikra zao wana mipango ya kuwaangamiza.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wiki hii sambamba na kusisitiza kwamba, ili Waislamu waweze kufikia saada na ufanisi wanapaswa kuwa macho amebainisha kwamba, watawala wa nchi za Kiislamu wakiwemo wa Aal Soud nchini Saudi Arabia hii leo wanatekeleza mipango michafu ya Marekani na utawala haramu wa Israel katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Ayatullah Kashani amesisitiza kwamba, watawala hao wanapaswa kufukuzwa kutoka katika nchi hizo za Kiislamu. Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, moja ya njama za maadui ni kutaka kuionyesha dini ya Kiislamu kwamba, haina muhtawa na kuongeza kuwa, maadui wakiwa katika njama za kufikia lengo hilo wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kuufasiri vibaya Uislamu.

Ayatullah Kashani ameashiria kukaribia kumbukumbu ya kutekwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran uliojulikana kama Pango la Ujasusi hapo Novemba 3, na kusisitiza kuwa, hii leo wananchi wa mataifa mbalimbali wakiwemo wa Yemen, Syria, Afghanistan, Iraq na Bahrain kama walivyo wananchi wa Iran, nao wamefikia natija hii kwamba, Marekani haina kitu kingine bighairi ya kufanya dhulma dhidi ya nchi nyingine.

3541346


captcha