IQNA

Iran yalaani mashambulio ya kigaidi katika miji ya Samarra na Tikrit Iraq

0:01 - November 07, 2016
Habari ID: 3470660
IQNA-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Iran amelaani hujuma za kigaidi iliyopelekea watu wasiopungua 24 kuuawa katika miji ya Samarra na Tikrit nchini Iraq siku ya Jumapili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi mbali na kutuma salamu za rambi rambi kwa familia za walipoteza maisha katika hujuma hizo , amesema jamii ya kimataifa ina jukumu la kukabuliana na ugaidi ulio dhidi ya ubinadamu wa makundi ya wakufurishaji.

Aidha amesema  wafanya ziara kadhaa Wairani wameuawa shahidi na wengine kujeruhiwa katika hujuma ya kigaidi ya Jumapili asubuhi mjini Samarra na kuongeza kuwa, jinai hiyo inatokana na  magaidi kushindwa katika medani za vita nchini Iraq.

Qassemi amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendele akuwa pamoja na serikali na watu wa Iraq hadi watakapopata ushindi kamili katika vita dhidi ya ugaidi.

Duru za habari zinadokeza kuwa wafanya ziara 7 Wairani wamepoteza maisha na wengine 47 kujeruhiwa katika hujuma ya kigaidi  mjini Samarra wakati basi lao lilipolengwa na bomu la magaidi.

Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limetangaza kutekeleza hujuma hiyo ya kigaidi. Serikali ya Iraq imetangaza kuchukua hatua kali zaidi za kulinda usalama hasa katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo imeanza kuwapokea mamilioni ya wafanyaziara wanaoelekea katika mji wa Karbala kwa ajili ya kumbukumbu ya Arobaini ya Imam Hussein AS.

3543888


captcha