IQNA

Qarii wa Misri asisitiza kujifunza Qur’ani utotoni

20:33 - November 12, 2016
Habari ID: 3470671
IQNA-Mwenyekiti wa Jumuiya ya Quraa (Wasomaji) wa Qur’ani Tukufu nchini Misri amesisitiza umuhimu wa kuwafunza watoto Qur’ani wakiwa wangali wachanga.

Katika mahojiano na Televisheni ya Misri, Sheikh Muhammad Mahmoud Tablawi amesema wazizi wanapaswa kujitahidi kuhakikisha kuwa watoto wao wanajifunza Qur’ani wakiwa bado katika umri wa chini.

Ameongeza kuwa suala la kuhifadhi Qur’ani miongoni mwa watoto linapaswa kupewa umuhimu mkubwa.

Kuhusu mojawapo ya mbinu za kusoma Qur’ani kwa sauti na lahni nzuri, amependekeza kujihusisha na riadha na mazoezi ili kuweza kupata pumzi ndefu kwa ajili ya qiraa bora.

"Binafsi, nilikuwa nacheza mpira na hilo lilinisaidia sana katika kupata pumzi ndefu wakati wa qiraa, kwani hii ni nukta muhimu kwa qarii wa Qur’ani,” ameongeza Sheikh Tablawi ambaye ana watoto 13.

Misri inajulikana katika Ulimwengu wa Kiislamu kama nchi yenye maqarii bora zaidi wa Qur’ani katika miongo ya hivi karibuni.

3545128

captcha