IQNA

Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Sharafeddin aaga dunia

10:50 - January 26, 2017
Habari ID: 3470814
IQNA: Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Muhammad Sharafeddin aliyepata umaarufu kwa mbinu yake ya Ibtihal ameaga dunia.
Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Sharafeddin aaga dunia

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Sharafeddin ambaye alikuwa na ulemavu wa macho, alipata umashuhuri kutokana na qiraa yake maridadi ya Qur'ani.

Aidha alikuwa akiwapenda Ahul Bayt wa Mtume SAW na pia alivutiwa sana na quraa Wairani pamoja na shughuli za Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kabla ya kuaga dunia, Sheikh Sharafeddin alisema alikuwa na hamu kubwa ya kutembelea Haram Takatifu ya Imam Ridha AS katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Hivi karibuni Kanali ya Televisheni ya Qur'ani nchini Iran ilikuwa imemualika Sheikh Sharafeddin ashiriki katika kipindi cha Golestan cha kanali hiyo.


3566016

captcha