IQNA

Qiraa ya Ibtihal ya Qarii Nasiruddin Toubar + Video

12:20 - May 09, 2022
Habari ID: 3475227
TEHRAN (IQNA)- Marhoum Sheikh Nasiruddin Toubar ni mashuhuri kwa qiraa ya Ibtihal katika ulimwengu wa Kiislamu.

Wakati wa uhai wake alirekodi qiraa kadhaa za Ibtihal ambazo ni za kiwango cha hali ya juu kwa mitazamo yote.

Sheikh Nasiruddin Toubar alizaliwa mwaka 1920 katika moja ya maeneo ya mkoa wa Dakahlia nchini Misri.

Katika zama za utoto wake alijifunza Qur'ani Tukufu, Ibtihal na Qasida. Sheikh Toubar alimuathiri Sheikh Mohammad Imran na hivyo kuwa na nafasi muhimu katika kuhuisha Ibtihal. Hatimaya aliaga dunia mwaka 1986 baada ya umri uliojaa baraka.

Kishikizo: Ibtihal ، sheikh toubar ، misri
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :