TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Madagascar imetangaza uamuzi wa kufunga madrassah na taasisi 16 za kufunza Qur'ani nchini humo hatua ambayo imewakasirisha Waislamu nchini humo.
Taarifa zinasema Wizara ya Elimu ya Madagascar imetumia kisingizio cha kukosekana suhula za kutosha kuwa sababu ya kufunga madrassa hizo za Qur'ani. Waziri wa Elimu katika nchi hiyo amezungumza kupitia radio ya taifa na kudai kuwa: "Taasisi hizi 16 awali zilianzisha kama madrassah binafsi za Kiislamu lakini hivi sasa zimegeuzwa na kuwa vituo vya kutoa mafunzo kamili na ya umma ya Qur'ani."