IQNA

Ongezeko la asilimia 57 la chuki didi ya Waislamu Marekani mwaka 2016

9:56 - May 11, 2017
Habari ID: 3470974
TEHRAN (IQNA)-Idadi ya vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu Marekani viliongezeka kwa asilimia 57 mwaka uliopita wa 2016.

Hayo yamedokezwa na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) katika ripoti iliyotangazwa Jumanne ambayo imeonyesha kukithiri chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Marekani.

Ripoti hiyo imedokezwa kwa mwaka jana kulikuwa na vitendo 2,213 dhidi ya Waislamu kote Marekani ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na vitendo 1,409 kama hivyo mwaka 2015.

Vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vinajumuisha hujuma dhidi ya misikiti, kushambuliwa Waislamu wanaotembea barabarani na ubaguzi katika maeneo ya kazi.

CAIR pia imesema Idara ya Polisi ya Upelelezi Marekani FBI imekuwa ikiwabugudhu Waislamu kwa kwa kuwasiliana nao mara kwa mara.

Taarifa ya CAIR inasema ingawa kulishuhudiwa ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu Markeani miaka ya nyuma, lakini kuibuka Donald Trump mwaka jana na hatimaye ushindi wake katika uchaguzi wa rais ni jambo ambalo limezidisha kwa kiasi kikubwa chuki dhidi ya Waislamu kutokana na misimamo yake ya kibaguzi dhidi ya Waislamu na wahajiri.


3462787
captcha