IQNA

Magaidi wafyatua risasi msikitini Ufaransa, Waislamu 8 wajeruhiwa

11:39 - July 04, 2017
Habari ID: 3471050
TEHRAN (IQNA)- Waislamu 8 wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi na magaidi mbele ya mlango wa msikiti kusini mwa Ufaransa.

Taarifa zinasema watu wenye silaha waliwafyatulia risasi Waislamu walipokuwa wakiondoka katika Msikiti waArrahma eneola Avignon Jumapili usiku.

Walioshuhudia hujuma hiyo imetekelezwa na watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao ambapo waliwafyatulia risasi Waislamu kiholela katika mlango wa msikiti na kuwajeruhi wanane akiwemo binti mwenye umri wa miaka saba.

Idara ya Mwendesha Mashtaka Ufaransa imedai kuwa, tukio hilo si la kigaidi na eti kwamba msikiti huo haukulengwa na kuongeza kuwa, ulikuwa ni mzozo baina ya vijana

Polisi wanasema hawajaweza kuwatambua washambuliaji hao na kwamba uchunguzi unaendelea.

Tukio hilo limeibua wasiwasi miongoni mwa Waislamu Ufaransa ambao hivi karibuni walisuhudia pia mtu moja akijaribu kuwakanyaga Waislamu kwa gari nje ya Msikiti wa Creteil a kusini mashariki mwa Paris.

Katika wiki za hivi karibuni bara Ulaya limeshuhudia vitendo kadhaa vya hujuma dhidi ya Waislamu. Katika siku kuu ya Idul Fitr mjini Newcastle nchini Uingereza,Waislamu sita waliokuwa wakiondoka msikitini baada ya sala ya Idi walijeruhiwa baada ya kugongwa kwa makusudi na gari la mtu mwenye chuki.

Halikadhalika katika msikiti wa Finsbury Park mjini London Mwislamu alipoteza maisha katika usiku wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya gari kuwagonga kwa makusudi Waislamu waliokuwa wakitoka katika Sala ya Tarawih. Aidha hivi karibuni pia mashariki mwa London Waislamu wawili walimiminiwa tindikali na watu wasiojulikana.

3463246

captcha