IQNA

Mashindano ya Qur’ani Ulaya kufanyika katika Siku Kuu ya Idul Ghadir

11:12 - August 06, 2017
Habari ID: 3471108
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur'ani Tukufu barani Ulaya yamepwanga kufanyika katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm kwa munasaba wa Siku Kuu ya Idul Ghadir.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika katika Kituo cha Kiislamu Cha Imam Ali AS mjini Stockholm Septemba 8-10.

Wasimamizi wanasema mashindano hayo yatafanyika chini ya uratibu wa Baraza la Mashindano ya Qur'ani la Ulaya Kaskazini, na kwamba mwaka huu, kutokana na maombi ya wasomaji wa nchi zingine za Ulaya, mashindano ya mwaka huu hayatajumuisha tu washiriki wa kaskaizni mwa bara hilo bali maeneo yote ya Ulaya. Aidha amesema mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur'ani, Adhana na ufahamu wa Qur'ani Tukufu.

Zahiri amesema mashindano hayo yanalenga kustawisha utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, umoja wa Waislamu na kutambua vipawa vya Qur'ani miongoni mwa Waislamu wa Ulaya. Halikadhalika mashindano hayo yatakuwa fursa kwa wanaharaakti wa Qur'ani kukutana na kubadilishana mawazo. Mashindano hayo yatasimamiwa na majaji wataalamu wa Qur'ani na washindi wanatazamiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwakani.

Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa na washiriki 92 kutoka Sweden, Norway, Denmark na Finland ambapo majaji walikuwa ni kutoka Denmark, Iran, Sweden, Ujerumani na Uholanzi.Mashindano ya Qur’ani Ulaya kufanyika katika Siku Kuu ya Idul Ghadir

Kuhusu Siku Kuu ya Idul Ghadir, inafaa kukumbusha hapa kuwa, tarehe 18 Dhulhija miaka 1428 iliyopita Mtume Muhammad (SAW) akiwa katika safari yake ya mwisho ya Hija, kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimtangaza Imam Ali bin Abi Twalib AS kuwa kiongozi wa Waislamu wote baada yake. Hatua hiyo ya Mtume Mtukufu ilifanyika katika eneo linalojulikana kwa jina la Ghadir Khum katika makutano ya njia ya Makka na Madina. Siku hiyo Mtume SAW alitoa hotuba mbele ya hadhara kubwa ya Waislamu kisha akashika mkono wa Ali bin Abi Twalib na kusema: "Kila mtu ambaye mimi ni kiongozi wake basi huyu Ali pia ni kiongozi wake. Mwenyezi Mungu ampende atakayempenda, na amfanyie uadui atakayemfanyia uadui." Mtume SAW pia aliwausia Waislamu kushikamana na Qur'ani na Ahlubaiti wake na akasema viwili hivyo havitatengana hadi vitakapomkuta yeye katika Hodhi ya Kauthar, Siku ya Kiyama.

3463556

captcha