IQNA

Kuzinduliwa Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran

14:51 - May 28, 2018
Habari ID: 3471534
TEHRAN (IQNA)- Kitengo cha kimataifa cha Maonyesho ya 26 ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kilizinduliwa Jumapili katika siku ya 11 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ufunguzi huo ulihudhuriwa na mabalozi wa nchi kadhaa za Kiislamu hapa nchini Iran, wanazuoni wa Qur'ani Tukufu na wanaharakati wa Qur'ani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Dkt. Mahmoud Vaezi, katibu wa kitengo cha kimataifa cha maonyesho hayo akihutubu katika uzinduzi huo alisema kitengo hicho kinalenga kuarifisha kimataifa  uwezo wa Iran katika masuala ya Qur'ani Tukufu.

Ameitaja Iran kuwa nchi inayoongoza duniani katika masuala ya Qur'ani kwa mitazamo mbali mbali.

Mabalozi wa Palestina na Algeria pia walihutubu katika hafla hiyo na kuwashukuru waandalizi kwa kuandaa mijumuiko ya Qur'ani yenye lengo la kuimarisha umoja wa Waislamu duniani.

Maonyesho ya 26 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalianza Mei 19 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA na hufanyika kila mwaka kwa muda wa wiki mbili katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3718144 

captcha