IQNA

21:38 - November 05, 2018
News ID: 3471730
TEHRAN (IQNA)- Awamu ya tatu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa wanawake yameanza Jumapili mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mashindano hayo ambayo rasmi yanajulikana kama  Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sheikh Fatima Bint Mubarak yanatazamiwa kuendelea hadi Novemba 16.

Ibrahim Mohamed Bu Melha, mshauri wa Mtawala wa Dubai katika masuala ya utamaduni amesema katika siku ya kwanza washiriki kutoka Cameroon, Iraq, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Ufilipino na Ubelgiji walishirik.

Mashindano hayo yanafadhiliwa na Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wa UAE na Mtawala wa Dubai.

Bu Melha amesema awamu hii ya mashindano ina washiriki kutoka nchi 63 katika kona zote za dunia. Mashindano hayo yanarushwa moja kwa moja au mubashara katika televisheni mbali mbali za UAE na pia kwa njia ya intaneti. Zahra Khalili mwenye umri wa miaka 12 anaiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo.

3467147

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: