IQNA

12:40 - April 24, 2019
News ID: 3471927
TEHRAN (IQNA)- Msichana mwenye umri wa miaka 19 na ambaye anaugua ugonjwa wa kupooza kwa ubongo (cerebral palsy) amefanikiwa kuhifadhi sura 42 za Qur'ani Tukufu.

Binti huyo, Sara al Balushi, amekuwa akisoma katika Kituo cha Qur'ani cha Mohammad bin Obaid huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kituo hicho, Nada Mohammad Obaid al Falasi, Al Balushi alianza kwa kuhifadhi sura tatu za An-Nas, Al-Falaq, Al-Ikhlas na Ayatul Kursi katika Surah Al Baqara akiwa na umri mdogo. Baada ya kujiunga na Kituo cha Qur'ani cha Mohammad bin Obaid, aliweza kuhifadhi surah 42 za Qur'ani na sasa anatumai kuhifadhi sura zote 114 Qur'ani Tukufu.
Al Falasi amesema kituo hicho huwasajili watoto wenye ulemavu wa ubongo na kimwili kwa sababu wao pia wana haki wa kuwa katika jamii. Amesema njia bora zaidi ya kuimarisha uwezo wa ubongo wa watoto kama hao ni kupitia kusoma na kuhifadhi Qur'ani.
Al Falasi pia ameishukuru familia ya Al Balushi, taasisi za Serikali ya Dubai na Shirika la Ambulanci la Dubai kwa msaada wao katika kuhakikisha kuwa Sarah anafika katika kituo hicho kujifunza Qur'ani.
3468364

Name:
Email:
* Comment: