IQNA

12:24 - May 20, 2019
News ID: 3471965
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai wametangazwa Jumapili usiku baada ya kuchuana kwa muda wa siku 12.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ambayo ni maarufu kama Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA), yamemalizika katika sherehe amayo imehudhuriwa na idadi kubwa ya maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mkurugenzi wa DIHQA, Ibrahim Mohammed Bu Melha ambaye pia ni mshauri wa Mtawala wa Dubai katika masuala ya utamaduni alimtangaza Muath Mahdmou Amir Bin Hamid wa Libya kuwa mshindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani na ametunukiwa zawadi ya Dh 250,000. Nafasi ya pili ilishikwa kwa pamoja na Ahmed Achiri wa Morocco na Ibrahim Maazou wa Niger. Nafasi zingine zilishikwa na Ahmed Bashir Aden, Marekani (4), Aymen Brahem, Tunisia (5), Omar Ahmad Hasan Aga (6), Syria, Abdelaziz Choukri, Algeria (7), Ahmed Mohamed Ibrahim, Kenya (7), Abdulla Khalifa Ebrahim Khalifa Hamdan, Bahrain(7), na Alsawi Abdullah Ahmad, Saudi Arabia (7).

Bu Melha amesema mashindano ya mwaka huu ambayo yalikuwa ya 23 yaliweza kuwavutia washiriki kutoka nchi 160.

3468561

Name:
Email:
* Comment: