IQNA

18:34 - May 27, 2019
1
News ID: 3471973
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kususia kongamano ambalo Marekani imeitisha nchini Bahrain ambalo Wapalestina wanamini kuwa linalenga kusambaratisha haki zao.

Wiki iliyopita Marekani ilitangaza itashirikiana na Bahrain kuwa mwenyeji wa kongamano litakalofanyika Juni 25-26 katika mji wa Manama kwa lengo eti la kuhimiza uwekezaji katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza ambao nao uko chini ya mzingiro.

Hatahivyo maafisa wa Palestina wanasema lengo kuu la kongamano hilo ni kuandaa mazingira ya utawala wa Rais Trump wa Marekani kuzindua kile ambacho kinatajwa kuwa ni 'Muamala wa Karne."

Katika taarifa Kamati ya Utendaji ya PLO imesema: "PLO inasisitiza msimamo wake wa mwisho wa kupinga kongamano hilo na haijatuma upande wowote kufanya mazungumzo kwa niaba ya watu wa Palestina."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa lengo la Marekani katika kongamano hilo ni kuanza kutekeleza mpango wa 'Muamala wa Karne na kuunganisha na uchumi baada ya kuchukua hatua za kutekeleza upande wa kisiasa wa mpango huo.

PLO imesema 'muamala wa karne' unalenga kuuimarisha utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na kufuta haki zote za kitaifa na kisheria za watu wa Palestina.

PLO imesisitiza kuhusu kupinga kikamilifu mpango huo tata wa Marekani na kusema itafungamana na haki za kisheria za Wapalestina.

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina pia nayo  imekosoa vikali mpango wa kufanyika mkutano wa Marekani wa kuzindua hatua ya mwanzo ya utekelezaji wa 'Muamala wa Karne' mwezi ujao wa Juni nchini Bahrain ikisisitiza kuwa kongamano hilo halina lengo jingine ghairi ya kuandaa mazingira ya kuimarisha na kufanya wa kawaida uhusiano kati ya Waarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

3468616

Published: 1
Under Review: 0
non-publishable: 0
OMAR ALIY
0
0
Tunajua nchi ya marekani na viongozi wake wote ni watu wanaopinga dini ya kiislamu na waislamu wote, pia hiyo wanashirikiana na nchi zilizo mkufuru mungu (israel), lengo lao ni kutaka kuuwangusha uislamu, ila hii haitowezekana kwasababu allah mtukufu alishaiongelea hali kama hii katika qur ani takatifu, natoa wito kwa kila muislamu duniani akemee na amuombe mungu ili azuie njia zao zote, na hakuna linaloshindikana kwa mungu so tunaamini hawatoweza kamwe.
Name:
Email:
* Comment: