IQNA

16:00 - November 08, 2019
News ID: 3472205
TEHRAN (IQNA) – Kwa mara ya kwanza katika Msikiti wa Blauwe huko Amsterdam Uholanzi, kumeadhiniwa wakati wa Sala ya Ijumma kwa kutumia vipaza sauti.

Kwa mujibu wa Imamu wa msikiti huo, Sheikh Yassin Elforkani, wataalamu wametumiwa kuweka vipaza sauti hivvo vyenye vipimo maalumu ili kuhakikisha kuwa Adhana haikiuki viwango vya sauti kwa mujibu wa sheria za mji wa Amsterdam. Sheikh Elforkani ameelezea matumaini kuwa, kuadhiniwa kwa kutumia vipaza sauti maalumu kutakuwa mwanzo wa sunna nzuri. Aidha amesema kuadhiniwa kwa vipaza sauti kutapelekea Uislamu uweze kuhisika  zaidi miongoni mwa wakaazi wa Amsterdam. "Hatutaki uchochezi bali tunataka mila na desturi za Kiislamu ziwe jambo la kawaida," ameongeza.

Msikiti wa Blauwe ni wa kwanza Uholanzi kutumia vipaza sauti maalumu kwa ajili ya Adhana. Awali Baraza la Mji wa Amsterdam lilipinga pendekezo hilo huku Meya Femke Halsema akisema Adhana haifai na imepitwa na wakati. Lakini baadaye walilazimika kukubali kuwa Adhana ni sehemu ya uhuru wa kuabudu, kama ambavyo makanisa ya Wakristo yanaruhusiwa kupiga kengele Jumapili na nyakazi zinginezo.

3469826

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: