IQNA

11:49 - November 27, 2019
News ID: 3472234
TEHRAN (IQNA) – Mufti wa Waislamu wa eneo la Volgograd Oblast nchini Russia amesisitiza ulazima wa kukombolewa mji Mtakatifu wa Quds, sehemu uliko Msikiti wa Al Aqsa na kusema kutetea Quds Tukufu na Palestina kunapaswa kuwa kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa.

Katika mahojiano na IQNA, Sheikh Kafa Muhammad Batan amelaani vikali hatua ya Wazayuni maghasibu kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa karibu kila siku. Msikiti wa al Aqsa ni kibla cha kwanza cha Waislamu na hivi sasa mji uliko msikiti huo yaani Quds (Jerusalem) unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Batan ambaye alikuwa Iran mapema mwezi huu kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu amesema maadui wa Uislamu wanajaribu kuwasahaulisha Waislamu kuhusu adui halisi kwa kuibua mifarakano baina yao.

Amesisitiza haja ya kuwepo umoja wa Waislamu ili kukabiliana na njama hizo za maadui za kuwagawanya.

Kwingineko katika mahojiano yake, Sheikh Batan amesema nchini Russia hivi sasa kuna harakati nyingi a Qur'ani na kwamba kuna mafunzo ya Qur'ani katika misikiti na vituo vya Kiislamu nchini humo.

Aidha amesema katika eneo la Volgograd Oblast kuna Waislamu 400,000 na sambamba na hilo kuna vituo vingi kwa Kiislamu.

Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulifanyika Novemba 14-12 mjini Tehran ambapo mada kuu katika mkutano huo ilikuwa ni 'Umoja wa Ummah katika kuutetea Msikiti wa Al Aqsa. Mkutano huo ambao hufanyika kwa munasaba wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW uliwaleta pamoja wasomi, wanazuoni, maulamaa, wanasiasa na wanafikra Wasialmu kutoka nchi 93.

3859433

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: