IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
19:33 - November 29, 2019
News ID: 3472240
TEHRAN (IQNA) -Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kulikuwa na mpango hatari nyuma ya wazua ghasia za hivi karibuni nchini Iran ambapo ghasia hizo ziliratibiwa na uistikbari wa dunia miaka miwili iliyopita sambamba na kugawa silaha na kutoa mafunzo.

Hujjatul Islam Wal Muslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari ameyasema hayo katika hotuba ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran ambapo akibainisha kuwa marekebisho ya bei ya mafuta nchini Iran kilikuwa kisingizio tu kilichotumiwa kwa ajili ya kuzua ghasia zilizoratibiwa na maadui, amesema kuwa, baada ya ubeberu wa dunia kushindwa mara kadhaa na mrengo wa muqawama unaoongozwa na Iran, ulijaribu kuingilia wimbi la malalamiko ya wananchi wa Iran ili kuielekeza nchi hii kwenye ghasia na vurugu. Akiashiria uungaji mkono wa kidiplomasia na kisiasa wa Marekani na kundi la kigaidi la Munafiqin (MKO) kwa wafanya ghasia nchini hapa amebainisha kuwa, katika machafuko ya hivi karibuni, wafanya ghasia waliwashambulia raia wa kawaida na maafisa usalama.

Amezidi kufafanua kuwa hata hivyo katika siku chache zilizopita raia wa Iran sambamba na kufanya maandamano makubwa ya kuunga mkono mfumo wa Kiislamu, wamesambaratisha njama zote za wafanya ghasia na maadui wa nchi hii. Akibainisha kuwa kusambaratika ubeberu wa dunia unaoongozwa na Marekani kunazidi kushuhudiwa siku hadi siku, Hujjatul Islam Wal Muslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari ameongeza kwamba, busara, uelewa wa mambo, kuona mbali, uimara na kujitolea kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kumesambaratisha njama zote za maadui.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni, wiki mbili ziliz, serikali ya Iran iliamua kukata ruzuku ya mafuta ya petroli iliyokuwa ikiitoa. Pamoja na kuondolewa ruzuku hiyo, bado Iran ni miongoni mwa nchi ambazo bei ya mafuta ya petrol ni ya chini zaidi duniani ambapo kwa sasa lita moja ya petroli kwa watumizi wa kawaida ni takribani senti 13 za Kimarekani. Maandamano ya kulalamikia hatua hiyo yalitumiwa vibaya na wahuni ambao waliibua ghasia na machafuko na kuteketeza mali ya umma na ya watu binafsi. Serikali ya Iran imetangaza kuwa fedha zitakazopatikana baada ya kuondolewa ruzuku zitatumika kuwasaidia watu wenye kipato cha chini katika jamii. Waziri wa Mafuta Iran Bijan Namdar Zanganeh amesema hatua ya kuongezwa bei ya amfuta ya petrol imepelekea kupungua matumizi ya bidhaa hiyo kwa lita milioni 20 kwa siku. 

3860314

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: