IQNA

Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa wa Ahul Sunna

Maadui wanalenga kuibua vita vya ndani nchini Iraq

11:35 - December 29, 2019
Habari ID: 3472313
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Ahul Sunna nchini Iraq amesema kuwa maadui wanalenga kuibua vita vya ndani na kuigawa nchi hiyo vipande vipande.

Katika mahojiano na Televisheni ya Al Mayadeen, Sheikh Khalid al-Mala, mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa wa Ahul Sunna nchini Iraq ameongeza kuwa, baadhi vya vyombo vya habari vimetumbukia katika mtano wa maadui na vinawachochea wananchi wanaoandamana wakabiliane na jeshi la nchi hiyo.

Aidha amepongeza jitihada za kuzuia machafuko ambazo zinatekelezwa na baadhi ya makundi ya kisiasa na pia Harakati ya Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufukama Hasdh al Shaabi.

Duru mpya ya maandamano nchini Iraq, ilianza Oktoba Mosi ambapo waandamanaji wanatka mabadiliko ili kuangamia ufisadi, ubadhirifu wa fedha za umma na matatizo ya kiuchumi. Maandamano hayo yametoa fursa kwa maadui kujipenyeza kwa lengo la kuileta madarakani serikali kibaraka wa Marekani.

Waziri Mkuu Adil Abdul-Mahdi kujizulu alilazimika kujiuzulia wadhifa wake lakini bado nchi hiyo haijaweza kupata waziri mkuu mpya.

Katika mchakato wa marekebisho ya kisiasa, Jumanne ya tarehe 24 Disemba, Bunge la Iraq lilipasisha sheria mpya za uchaguzi nchini humo ambazo ni majumui ya vipengee 50. Kufanyiwa mabadiliko sheria za uchaguzi, kuweko marekebisho ya katiba, kuuzuliwa Waziri Mkuu na kuundwa serikali mpya ndio yaliyokuwa matakwa ya wananchi wa Iraq waliokuwa wakiandamana katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

3867243

 

captcha