IQNA

Magazeti ya Uingereza yanapotosha kuhusu Uislamu

13:31 - December 30, 2019
Habari ID: 3472317
TEHRAN (IQNA) – Magazeti nchini Uingereza vimekuwa vikiwasilisha taswira mbaya na potovu kuhusu Uislamu na Waislamu.

Hayo yamesemwa na Alan Moses mwenyekeiti anayeondoka wa Taasisi Huru ya Viwango vya Vyombo vya Habari Uingereza (IPSO) ambaye amesema: "Haya ni maoni yangu binafsi. Mara kwa mara vyombo vya habari huandika kuhusu Waislamu kwa namna ambavyo haviwezi kuthubuti kuandika kuhusu Mayahudi au Wakatoloki."

Kauli hiyo inakuja wakati ambao IPSO inakaribia kuchapisha muongozo kwa waandishi habari kuhusu nukta za kuzingatia wakati wa kuripoti kuhusu Waislamu, ambao ni takribani asilimia 5 ya watu wote wa Uingereza.

Uamuzi huo unakuja baada ya kamati maalumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza kubaini kuwa kuna ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika vyombo vya habari, hasa magazeti, ambapo IPSO ilituhumiwa kwa kutotoa muongozo kuhusu kukabiliana na upotoshaji katika magazeti.

IPSO ilibuniwa mwaka 2014 na inasimamia magazeti aidi ya 1,000 Uingereza na inauwezo wa kulazimu gazeti kurekebisha au kulipa faini baad aya kuandika habari zenye kupotosha ukweli wa mambo.

Miqdaad Versi, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Uislamu la Uingereza anasema hata kama baadhi ya magazeti yanarekebisha habari potovu zilizoandikwa lakini ni nadra kuona taarifa ya marekebisho ikipewa kipaumbele sawa na ile habari ya awali ya upotoshaji.

3867560

captcha