IQNA

Jaji wa kwanza Muislamu mwenye kuvaa Hijabu Uingereza

22:49 - May 23, 2020
Habari ID: 3472794
TEHRAN (IQNA)- Jaji wa kwanza Muislamu mwenye kuvaa Hijabu ameteuliwa katika mfumo wa mahakama nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa Bi.  Raffia Arshad ameanza kazi rasmi kama mwanamke wa kwanza Muislamu mwenye kuvaa Hijabu ambaye ni jajji katika mfumo wa mahakama nchini Uingereza.

Bi. Arshad ameteuliwa kuwa naibu jaji katika eneo la Midland Circuit  nchini Uingereza. Jaji Mkuu wa Uingereza amesema uteuzi wa Raffia utachangia kuongeza anuai ya watu wanaohudhumu katika mfumo wa mahakama.

Bi. Arshad ni mtaalamu wa kanuni za familia na sheria ya Kiislamu.

Leo Waislamu wanaoishi Uingereza wanatoka mataifa mbali mbali duniani huku kukiwa na idadi kubwa ya Waingereza waliosilimu. Pamoja na mchango wao mkubwa na wa kihistoria, Waislamu Uingereza wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa kubaguliwa na kutengwa na watu wenye misimamo mikali ya utaifa na chuki dhidi ya Uislamu.

wa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. 

/3900954

captcha