IQNA

19:27 - January 07, 2020
News ID: 3472351
TEHRAN (IQNA) –Wananchi wa Nigeria wameshiriki katika maandamano ya kulaani jinai ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis.

Katika maandamano yaliyofanyika katika miji mbali mbali ya Nigeria, wananchi walisikika wakisema: "Sisi Sote ni Soleimani, Sisi Sote ni Abu Mahdi".

Aidha Waislamu wa Nigeria pia wametoa nara za 'Mauti kwa Marekani' huku wakilaani ugaidi wa Marekani katika kuwaua makamanda hao wawili wa Iran na Iraq na wanajihadi wengine waliokuwa wameandamana nao. Maandamano hayo yamefanyika katika miji kama vile mji mkuu Abuja, Katsina na Kano.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria aidha imetoa tamko na mbali na kuilaani Marekani kwa kumuua kigaidi Kamanda Qassem Soleimani, imelipa mkono wa pole taifa na serikali ya Iran na kusisitiza kuwa, ugaidi huo wa Marekani ni jinai isiyosameheka.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine nane, walishambuliwa kwa anga na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote walikufa shahidi katika tukio hilo.

3868880

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: