IQNA

20:13 - January 17, 2020
News ID: 3472380
TEHRAN (IQNA) - Idadi kubwa ya wananchi waumini wa Iran wamefanya maandamano makubwa katika kuunga mkono mfumo wa Kiislamu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kusimama kidete katika kukabiliana na ya Marekani.

Maandamano hayo ambayo famefanyika katika miji tofauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamejiri baada ya kumalizika kwa Swala ya Ijumaa ambapo washiriki sambamba na kulaani jinai za kila mara za serikali ya Marekani na uingiliajia wa Uingereza katika masuala ya ndani ya Iran, wametangaza uungaji mkono wao kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC. Aidha baada ya maandamano hayo, wananchi wa Iran wametoa azimio ambalo limeashiria chanzo kikuu cha uadui wa Marekani na Uingereza dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, na kutaka kuhitimishwa uingiliaji wa masuala ya ndani ya Iran unaofanywa na nchi hizo. Katika azimio hilo wananchi wa Iran wamesisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefikia hatua ya kujitegemea, kusimama imara na uwezo mkubwa ambapo mbali na kukataa moja kwa moja ubeberu au kukubali kuwa chini ya ubeberu huo, wamesema kuwa taifa hili limetoa kipigo angamizi dhidi ya maadui na ubeberu wa kimataifa kupitia vita vikubwa katika nyuga tofauti za kisiasa, vyombo vya habari, kiuchumi na kijeshi, na hivyo kuweza kufelisha njama za udhibiti wa Marekani, Uingereza na utawala haramu wa Kizayuni na washirika wao.
Azimio hilo pia limeashiria kusimamishwa meli ya Uingereza, kuangamizwa ndege ya ujasusi ya Marekani na pia kushambulia kwa makumi ya makombora kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq, kuwa ni sehemu ya fakhari na izza ya Iran katika kukabiliana na uistikbari wa dunia. Kadhalika raia wa Iran wametangaza uungaji mkono wao kwa hatua ya kujitolea nafsi majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama ambavyo pia wametangaza uungaji mkono wao wa pande zote kwa muqawama wa Kiislamu katika kukabiliana na njama za Marekani na kulitaja suala hilo kuwa jukumu lao kibinadamu na kidini.

3872254

Name:
Email:
* Comment: