IQNA

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard
21:29 - January 24, 2020
News ID: 3472403
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa mauaji yaliyofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani dhidi ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni mwanzo wa kufukuzwa Marekani katika eneo hili la magharibi mwa Asia sambamba na washirika wake katika eneo kusambaratika.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard pia amezungumzia mahudhurio makubwa ya mamilioni ya wananchi wa Iraq katika maandamano ya leo Ijumaa mjini Baghdad wakitaka kuondoka jeshi la Marekani nchini humo na kusema: Kwa maandamano hayo adhimu, wananchi mashujaa wa Iraq wametengeneza hamasa kubwa na kujiunga na mataifa mengine ya Waislamu wa kanda hii wanaopiga nara na kaulimbinu ya "Mauti kwa Marekani". Halikadhalika amesema kuwa shambulizi la makombora la Iran dhidi ya kambi za jeshi vamizi la Marekani nchini Iraq limeporomosha uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo.
Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard ameashiria mahudhurio makubwa ya wananchi wanamapinduzi na Waislamu wa Tehran katika Swala ya Ijumaa ya wiki iliyopita iliyoongozwa na Ayatullah Ali Khamenei na kusema: Kupitia mahudhurio hayo makubwa, kwa mara nyingine tena taifa la Iran limeonesha mfungamano wake imara na Kiongozi wa Mapinduzi, thamani na malengo ya Imam Khomeini na mashahidi.
Khatibu wa Swala ya leo ya Ijumaa mjini Tehran pia ametilia mkazo udharura wa kuwepo umoja na mshikamano baina ya mataifa ya Waislamu kwa ajili ya kukabiliana na njama za Marekani.

3873791

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: