IQNA

Khatibu : Ushirikiano wa Iran, Russia na China ni kwa ajili ya usalama wa Asia

19:18 - January 21, 2022
Habari ID: 3474832
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaandaa ramani ya njia ya ushirkiano na nchi zingine kwa kuzingatia maslahi yake ya taifa.

Hujjatul-Islam Sayyid Mohammad Hossein Abu Turab Fard  ameashiria mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya vikosi vya wanamaji wa Iran, Russia na China na akasema: mazoezi kama haya ya pamoja yanaweza kutoa mchango katika kuinua kiwango cha usalama wa eneo na pia ni kiashiria cha mabadiliko muhimu katika mustakabali wa eneo.

Abu Turabi amesema, kwa mtazamo wa wananadharia wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, milenia ya tatu ni milenia ya  Asia na akafafanua kwamba, kutokana na kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu katika sayari ya dunia, bara la Asia lina nafasi muhimu sana na ya kipekee.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran, vilevile amegusia uwezo wa nishati uliopo katika bara la Asia na akasema, "leo bara hili lina nafasi na sauti ya juu, kwa kuwa kitovu kikuu cha uzalishaji nishati duniani."

Halikadhalika, Hujjatul-Islam Sayyid Mohammad Hossein Abu Turab Fard amezungumzia safari Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Seyyid Ebrahim Raisi nchini Russia na akaeleza kwamba, kuimarisha uhusiano na nchi hiyo jirani kwa kuzingatia manufaa na maslahi ya taifa ya nchi ya Iran, ambayo leo hii ni dola lenye nguvu na limesimama imara kwa muda wa miongo minne kukabiliana na watumaji mabavu, kunaweza kuwa na mchango muhimu katika kuinua kiwango cha usalama wa eneo pia.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza kuwa, tajiriba ya Iran ya kukabiliana na ubeberu wa Marekani inaweza kutoa msukumo kwa ushirikiano wa Iran, Russia na China kwa jili ya kuimarisha usalama wa Asia.

4030134

captcha