IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Iran ina uwezo wa kiulinzi za kulinda amani kieneo na Ulimwengu wa Kiislamu

19:54 - February 18, 2022
Habari ID: 3474942
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mingoni mwa nchi chache zenye nguvu za kiulinzi za kudhamini amani na usalama wa eneo na wa Ulimwengu wa Kiislamu.

Hujjatul-Islam Mohammad Hossein Abu Turabi Fard amebainisha kuwa, nguvu na uwezo mkubwa wa kisiasa, kiulinzi, kiutaalamu na wa kiusalama pamoja na hadhi ya kujivunia iliyonayo Iran katika Ulimwengu wa Kiislamu, sambamba na kuchanua fikra za Uislamu asilia ni matunda ya kushikamana na misingi miwili mikuu ya ustawi na maendeleo, ambayo inapasa izidi kupewa umuhimu na viongozi waandamizi, wa ngazi ya chini pamoja na jamii nzima.

Halikadhalika, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, uwezo, nguvu na mafanikio uliyopata Mfumo wa Kiislamu katika eneo, ulimwenguni na ndani ya Iran ya Kiislamu katika miongo minne iliyopita yametokana na hatua zilizopigwa katika njia ya ustawi na maendeleo na akaongeza kwamba, matunda ya utawala na uongozi wa Kiislamu ni kuandaliwa na kupatikana watu walioweza kufikia vilele vya elimu na taaluma na kuwezesha jamii kuishi maisha ya kimaada yanayozingatia maadili mema.

Hujjatul-Islam Abu Turabi Fard ameashiria pia hotuba ya jana ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei katika hadhara ya watu wa Tabriz na akasema, katika maagizo aliyotoa, Kiongozi Muadhamu alitilia mkazo juu ya nukta hiyo, ya kwamba inapasa kustawisha miundomsingi ili kufikia lengo la kujenga Ustaarabu wa Kiislamu na kukwea hadi kwenye vilele vyake.

4037118

captcha