IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijuma Tehran
22:32 - January 31, 2020
News ID: 3472425
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ameilaani Marekani kwa kuanzisha njama mpya dhidi ya Waislamu kwa jina la "Muamala wa Karne" na kusema kuwa, njama hizo zitafeli na kushindwa tu.

Jumanne usiku, rais wa Marekani, Donald Trump akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alizindua rasmi mpango huo wa kibaguzi wa eti "Muamala wa Karne."

Miongoni mwa vipengee viovu kabisa vilivyomo kwenye njama hizo mpya za Marekani ni kutambuliwa Baytul Muqaddas kuwa eti mji mkuu wa Israel, kupewa Wazayuni asilimia 30 ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kupigwa marufuku Wapalestina kurejea katika ardhi za mababu zao na kupokonywa silaha kikamilifu makundi ya muqawama ya Palestina.

Akikosoa na kulaani vikali njama hizo, Ayatullah Mohammad Ali Movahedi Kermani, Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema katika khutba za leo za sala hiyo kwamba, kimsingi mpango wa "Muamala wa Karne" ni "Kashfa ya Karne" ni "Udhalilishaji wa Karne" na ni "Usaliti wa Karne." Ameongeza kuwa, muamala huo wa rais wa Marekani, Donald Trump ni matunda ya usaliti wa baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu lakini hakuna njama wala usaliti wowote unaoweza kupoteza haki za wananchi wa Palestina.

Amesema, wapenda haki wote duniani wamezilaani njama hizo za muamala wa karne na kwamba kambi ya muqawama itaivunja mshipa wa shingo Marekani na kuikomboa Palestina.

Waislamu waliomiminika kwenye Sala ya Ijumaa leo hapa Tehran wamepiga nara za kulaani njama hizo mpya za Marekani na kutangaza uungaji mkono wao kamili kwa taifa la Palestina.

3875385

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: