IQNA

20:30 - March 29, 2020
News ID: 3472614
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameashiria vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: Madaktari na wananchi wa Iran daima wamekuwa wakifanya mambo yanayolipa fahari taifa hili na sasa wanapata mafanikio katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 au corona na kusimamia vyema masuala ya nchi.

Rais Hassan Rouhani ambaye mapema leo alikuwa akizungumza kwenye kikao cha baraza la mawaziri mjini Tehran na kuongeza kuwa, ripoti iliyotolewa na Waziri wa Afya hapa nchini kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19  inaonyesha kuwa, Iran iko kwenye nafasi inayokubalika katika kutibu na kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.

Amebaini kuwa mikoa mingi hapa nchini imevuka kipindi cha mlipuko wa maambukizi ya corona na kuongeza kuwa: Ulinganisho wa takwimu na ripoti za maambukizi ya corona nchini Iran na takwimu za nchi nyingine na hata nchi za Ulaya na za Magharbi, unaonyesha kuwa, hali ya Iran ni bora za nzuri zaidi ikilinganishwa na ya nchi hizo.

Rais Rouhani amewataka wananchi wajitayarishe kwa ajili ya kipindi cha baada ya corona na kusema: Uzalishaji, afya, na usalama wa wananchi ni nguzo muhimu nchini Iran ambazo daima zinapewa kipaumbele na serikali.

Hadi sasa Wairani 38,309 wamepatwa na virusi vya corona. Wagonjwa 2,640 kati yao wameaga dunia na zaidi ya 12,391 wamepata nafu na kupona.

3888009/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: