IQNA

17:09 - March 28, 2020
News ID: 3472609
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kukabiliana ugonjwa wa COVID-19 au corona, ni lazima kutekelezwa kikamilifu na kwa uangalifu mpango wa 'kutokaribiana watu' (social distancing) nchini Iran.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo Jumamosi katika kikao cha kamati ya kitaifa ya kusimamia na kukabiliana na virusi vya Corona mjini Tehran na kuongeza kuwa, kupitishwa mpango huo wa kutokaribiana watu wanapokuwa sehemu moja utaendelea hadi tarehe 20 Farvardin inayosadifiana na tarehe 8 Aprili. Amefafanua kuwa watu wote na vyombo vya utekelezaji nchini Iran ni lazima viwe na ushirikiano katika kukabiliana na Corona. Aidha kwa mara nyingine Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa Iran wako katika mazingira magumu ya vikwazo na dunia inaendelea kushangazwa ni namna gani nchi ambayo iko chini ya vikwazo imeweza kusimama imara katika kukabiliana na virusi angamizi vya corona.

Tangu mwanzo kuliporipotiwa virusi vya corona nchini Iran, kulianza kutekelezwa hatua za kuzuia na za matibabu kwa msaada wa jeshi na vyombo vyote husika na hadi sasa hatua za kuwatenga wagonjwa (kuwaweka karantini) na kuwatibu waathirika wa corona zingali zinaendelea kutekelezwa kwa haraka kupitia ushirikiano wa watu wote. Mpango wa kuweka utengano wa kijamii ambao pia una lengo la kukata msururu wa kusambaa maradhi hayo, kupitia kuzuia mikusanyiko na kufuta safari zote zisizo za dharura nchini, ulianza kutekelezwa Ijumaa asubuhi.

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya 600,000 wameambukizwa COVID-19 duniani, wengi wao wakiwa Marekani huku na miongoni mwao walioaga dunia ni 27,417 wengi wao wakiwa nchini Italia.

Nchini  Iran walioambukizwa COVID-19 ni 35,408 huku 2,517 wakipoteza maisha na wengine 11,133 wamepata nafuu na kuruhusia kuenda nyumbani baada ya kulazwa hospitalini.

3887786

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: