IQNA

Kwa mara ya kwanza duniani

Iran yazindua kifaa erevu cha kugundua kilipo kirusi cha corona

12:18 - April 16, 2020
Habari ID: 3472670
TEHRAN (IQNA) - Kwa mara ya kwanza duniani, Jamhuri ya Kislamu ya Iran imevumbua kifaa chenye uwezo wa kugundua mwili na sehemu kilipo kirusi cha corona katika umbali wa mita 100 tena katika kipindi cha sekunde chache tu. Kifaa hicho kimepewa jina la "Musta'an 110."

Kifaa hicho kilizinduliwa jana Jumatano kwa mara ya kwanza katika sherehe zilizohudhuriwa na Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, jeshi ambalo liko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya corona nchini Iran. 

Kamanda Mkuu huyo wa jeshi la IRGC amesema kwenye sherehe hizo kwamba, teknolojia hiyo mpya ina uwezo wa kugundua maeneo na watu walioambukizwa corona katika kipindi cha sekunde chache tu. Ni teknoljia mpya kabisa ambayo imevumbuliwa na wanasayansi wa jeshi la kujitolea la Basiji. Amesema, kifaa hicho kinatumia teknolojia mpya, ya kisasa na ya kipekee

Wataalamu wa IRGC wanasema kifaa hicho kipya hakihitajii kuchukua vipimo vya damu, bali kinaweza kugundua maeneo na watu walioambukizwa korona katika masaha ya hadi mita 100 na tayari kimeshafanyiwa majaribio mengi mahospitalini na kimekuwa na matokeo mazuri kwa asilimia 80. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu kifaa hicho kipya, Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema, huu ni uvumbuzi mpya wa sayansi na teknolojia na ni wa kipekee. Ni teknolojia iliyovumbuliwa na wanasayansi wa jeshi la kujitolea la Basiji katika kipindi hiki kifupi cha kuenea corona humu nchini. Ni kifaa ambacho kinaweza kuongozwa kwa mbali na kinaweza kutumika si kwa ajili ya kugundua kirusi cha corona tu, bali pia jamii nyingine za virusi.

Aidha amesema chombo hicho kinatumika katika oparesheni za kupuliza dawa kwenye maeneo mbalimbali ili kuua virusi vya corona na hivyo hakutakuwa na haja ya kupuliza dawa katika maeneo yasiyo na  virusi.

Meja Jenerali Salami amesema chombo hicho kimefanyiwa majaribio katika mahospitali nchini Iran na uwezo wake wa kufanya kazi bila makosa ni asilimia 20 huku akiongeza kuwa watazidi kukiboresha ili kifanye kazi kwa njia bora zaidi.

3891844

captcha