IQNA

Msimamo wa Iran kuhusu yanayojiri nchini Yemen

11:05 - April 30, 2020
Habari ID: 3472717
TEHRAN (IQNA) -Sayyed Abbas Mousawi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa njia pekee ya kurejesha uthabiti na utulivu Yemen ni umoja na mshikamano miongoni mwa makundi mbali mbali nchini humo.

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono kudumishwa umoja na mshikamano wa maeneo yote ya Yemen.

Mousavi ameashiria matukio ya hivi karibuni ya kutaka kuigawa Yemen vipande vipande na kusema: " Hatua kama hizo si tu kuwa haziwezi kutatua matatizo ya sasa ya Yemen bali yatafanya hali ya nchi hiyo kuwa mbaya zaidi.

Baraza la Mpito la kusini mwa Yemen ambalo linapata uunga mkono wa Umoja wa Falme za Kiarabu Jumapili lilitangaza kuwa mikoa ya kusini mwa Yemen itakuwa na serikali zenye mamlaka ya kujitawala.

Baraza hilo aidha lilitangaza hali ya hatari katika maenei hayo ya kusini kuanzia Jumamosi.

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani hatua ya wanamgambo wanaopata himaya ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kujitangazia uhuru huko kusini mwa Yemen na kusema kuwa, hatua hiyo ni kutangaza kujitoa kikamilifu wanamgambo hao katika makubaliano ya Riyadh kati yao na serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabbuh Mansour Hadi.

Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen ambaye ni katika viongozi wa ngazi za juu wa harakati ya Answarullah ameiambia serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabbuh Mansour Hadi kwamba, nyinyi muda wote mumekuwa mukidai kuwa eneo la kusini mwa Yemen liko mikononi mwenu, haya sasa tekelezeni makubaliano chapwa ya Riyadh na wazuieni wanamgambo wa Imarati kujitangazia uhuru kusini mwa Yemen.

3895352

captcha