IQNA

Majeshi ya Iran yako tayari kuzisaidai nchi za eneo katika vita dhidi ya corona

15:28 - May 02, 2020
Habari ID: 3472725
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuyanufaisha mataifa mengine uzoefu wake katika suala la kupambana na ugonjwa wa corona au COVID-19.

Meja Jenerali Muhammad Hossein Baqeri amesema hayo leo Jumamosi katika barua alizowatumia  kwa nyakati tofauti Mawaziri wa Ulinzi na Wakuu wa Kamandi za Vikosi vya Ulinzi wa nchi za Iraq, Jamhuri ya Azerbaijan, Afghanistan, Pakistan, Oman, Qatar, Kuwait, Syria na Lebanon.

Katia barua hizo amegusia mafanikio makubwa iliyopata Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupambana na maambukizi ya corona, amezungumzia pia mchango mkubwa wa vikosi vya ulinzi humu nchini katika kukabiliana na kirusi hatari cha corona. Amesema, vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kuzipatia nchi rafiki uzoefu vilioupata katika kupambana na ugonjwa huo.

Mkuu huyo wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran amesisitiza kuwa, kutopambana kwa njia sahihi na kiutalaamu na ugonjwa wa corona kunaweza kuongeza kasi ya kuenea ugonjwa huo na kuutia hatarini usalama wa taifa zima. Ameongeza kuwa, mafanikio iliyopata Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupambana na kuudhibiti ugonjwa wa COVID-19 ni fursa nzuri kwa mataifa mengine ya Kiislamu na nchi marafiki na jirani na Iran, ya kuweza kupambana vilivyo na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa corona ambao jina lake rasmi na COVID-19 uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan, China, mwishoni mwa mwaka 2019 na hivi sasa umeshaenea katika nchi zote duniani. Idadi ya watu waliokuwa wameshaambukizwa corona kote duniani kufikia Mei 2 2020 asubuhi ilikuwa ni 3,402,034 (milioni tatu na laki nne na elfu na 34). Kati ya hao watu 1,083,908 (milioni moja na 83 elfu na 908) walikuwa wameshapona na 239,622 walikuwa wameshafariki dunia.

3895753

captcha