IQNA

Wageni waalikwa kutembelea misikiti Uingereza kwa njia ya intaneti + Video

23:29 - June 18, 2020
Habari ID: 3472877
TEHRAN (IQNA)- Mpango wa kila mwaka wa kuwaalika wasiokuwa Waislamu kutembelea misikiti nchini Uingereza mwaka huu umefutwa kutokana na kuibuka ugonjwa wa COVID-19 lakini pamoja na hayo kumezinduliwa mpango wa kutembelea misikiti kupitia intaneti.

Baraza la Waislamu Uingereza (MCB)  katika kipindi cha miaka mitnao sasa limekuwa na mpango wa kila mwaka wa kuwaalika wasiokuwa Waislamu kote Uingereza kutembelea misikiti ili kujifunza kuhusu Waislamu na Uislamu na hiyo kuondoa taswira potovu zilizoko.

Mwaka huu kutokana na kuibuka COVID-19 na kufungwa misikiti katika maeneo mengi, wasiokuwa Waislamu wamealikwa kutembelea misikiti kwa njia ya intaneti yaani virtual tour.

Haroun Khan Katibu Mkuu wa MCB pia amesema mwaka huu pia kutokana na kuwa watu hawawezi kufika misikitini, baadhi ya misikiti inatekeleza mpango wa kuwasambazia chakula watu wasiojiweza pamoja na kuwapa huduma za kiafya hasa katika kipindi hiki cha janga la COVID-19.

3905525

captcha