Kwa mujibu wa taarifa, makumi ya maelfu ya Wapalestina walisafiri hadi mji Jumapili asubuhi za mapema, wakiwa na nia ya kuhudhuria Swala hii muhimu inayoashiria kufika ukingoni mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mamlaka za Israel zilikuwa zimetekeleza mfululizo wa vikwazo, ikiwa ni pamoja na vizuizi vya umri, ili kuzuia wakaazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi , Mashariki mwa al-Quds, na maeneo mengine kufika katika Msikiti wa Al Aqsa.
Idadi kubwa inaonyesha jitihada zinazoendelea za Wapalestina kuhakikisha wanatekeleza ibada katika Al-Aqsa, licha ya changamoto zilizowekwa na vikwazo vya Israeli.
Katika taarifa iliyotolewa kabla ya sikukuu, Harakati ya Palestina ya Mapambano ya Kiislamu ,Hamas, ilikuwa imewahimiza Wapalestina kusafiri hadi Msikiti wa Al-Aqsa, kushiriki katika ibada, na kupinga udhibiti wa Israel juu ya eneo hilo. Taarifa hiyo ilihimiza mshikamano unaoendelea na Gaza, Al-Quds, na Msikiti wa Al Aqsa.
Sheikh Ekrima Sabri, mhubiri wa Msikiti wa Al-Aqsa, pia aliwasihi Wapalestina kukusanyika katika msikiti huo kama ishara ya upinzani dhidi ya juhudi za mamlaka za Israeli za kuzuia ufikiaji wa Wapalestina kwenye eneo hilo la tatu kwa utakatifu katika Uislamu.