IQNA

Malaysia kutumia mbinu za kulinda mazingira ili kuzuia israfu

22:45 - September 28, 2020
Habari ID: 3473211
TEHRAN (IQNA) – Misikiti zaidi Malaysia imejiunga na ‘Mpango wa Msikiti wa Kijani’ unaohusu kuzuia kulinda mazingira katika matumizi ya maji na umeme.

Mkurugenzi wa Kituo cha Tekenolojia ya Kijani na Mabadiliko ya Hali ya Hewa Malaysi (MGTC) Shamsul Bahar Mohammad Nor  amesema mbinu hiyo  ya kulinda mazingira itapelekea kupungua israfu na hivyo kuokoa gharama za matumizi ya maji na umeme misiktini. Amesema mbinu hiyo itawanufaisha wote katika jamii. Kati ya mbinu hizo zinazotumiwa ni kutegemea umeme wa miale ya jua au sola ambapo misikiti itaweza kuokoa asilimia 40 ya bili za umeme.

Aidha mpango huo utajumuisha pia urejelezaji maji  (water recycling) sambamba na kutoa elimu ya kutunza mazingira.  Waziri wa Mazingira na Maji nchini Malaysia Ibrahin Tuan Man amesema misikiti 10 itashiriki katika mpango huo kama hatua ya awali ya majaribio. Aidha amesema katika siku za usoni misikiti itajengwa kwa kuzingatia mbinu hizo za uzuiaji israfu na utunzaji mazingira katika matumizi ya maji na umeme.

Mwaka 2017, nchini jirani ya Indonesia, nayo ilitangaza mpango wa kuzindua misikiti 1,000 ya 'kijani' kwa maana kuwa kwa maana kuwa ujenzi na utumizi wake umezingatia utunzwaji mazingira.

Makamu wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla alisema misikiti hiyo inajengwa kwa kuzingatia  kuwepo nishati jadidika, kuzuia israfu katika utumizi wa maji na pia kuwepo urejelezaji maji.

Katika Umoja wa Falme za Kiarabu pia kumezinduliwa msikiti erevu (smart mosque) katika eneo la Ras Al Khaimah. Kwa mfano maji yanayotumiwa kwa ajili wa wudhuu hutumiwa tena baada ya kusafishwa kwa mashine maalumu zilizo hapo na kutumika kwa ajili ya mimea au bustani ya msikiti. Aidha anasema taa za msikiti huo zinatumia nishati ya jua na huwaka na kujizima zenyewe kwa kuzingatia wakati wa Sala na idadi ya waumini ndani ya msikiti. 

/3472650

Kishikizo: malaysia ، msikiti
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :