IQNA

Hamas: Ujumbe wa kiongozi wa Iran unaashiria himaya ya kudumu kwa malengo ya Palestina

22:07 - July 06, 2020
Habari ID: 3472935
TEHRAN (IQNA) –Mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amepongeza ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na kusema: “ Ujumbe wa kiongozi wa Iran unaashiria himaya ya kudumu kwa malengo ya Palestina.”

Katika mahojiano na televisehni ya Al Mayadeen, Ismail Ridhwan amesema: “Kiongozi Muadhamu wa Iran katika ujumbe wake kwa Haniya amesisitiza kuhusu kuunga mkono taifa la Palestina na mapambano au muqawama.”

Ameongeza kuwa:  “Ujumbe wa Ayatullah Khamenei unaashiria uungaji mkono wa kistratijia kwa taifa la Palestina na pia unaashiria uungaji mkono usio na kikomo kwa malengo matukufu ya Palestina.”

Afisa huyo wa ngazi wa Hamas ambaini kuwa, ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ni fahari kubwa na kuongeza kuwa: “Sisi tutaendeleza njia ya muqawama.”

Ismail Ridhwan amesema msimamo imara wa kuunga mkono taifa la Palestina umewapa matumaini Wapalestina kuhusu mustakabali.

Halikadhalika amesema mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kunyakua zaidi ardhi za Palestina katika Ukingo wa Magharibi hautafanikiwa na kwamba harakati za ukombozi wa Palestina zimeweka machaguo yote mezani.

3909066

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha