IQNA

"Allahu Akbar" yasikika katika maandamano ya kupinga ubaguzi Marekani +Video

10:20 - July 09, 2020
Habari ID: 3472943
TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi Marekani walisikika wakitamka Takbir yaani Allahu Akbar.

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi Marekani yanaandelea nchini Marekani kufuatia mauaji ya kinyama ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd.

Itakumbukwa kuwa, mnamo Mei 25, afisa wa polisi katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesta nchini Marekani alimbinya shingo kwa kutumia goti kwa dakika 9 hivi George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika hadi akakata roho.

Muaji hayo ya kikatili chini ya kaulimbiu ya "Siwezi kupumua" matamshi yaliyosikika yakitoka kinyonge kinywani mwa Floyd alipokuwa akiuawa, yanaendelea kushuhudiwa ndani na nje ya Marekani.

Tokea wakati huo Wamarekani wamekuwa wakiandamana karibu kila siku kwa lengo la kulaani ubaguzi wa kiserikali huku wakitaka haki kwa wote hasa watu wa jamii za waliowachache.

3909459

Kishikizo: marekani ، takbir ، George Floyd
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha