IQNA

Rais Hassan Rouhani

Kubinya shingo kwa kutumia goti ni sera ya daima ya Marekani

22:27 - June 10, 2020
Habari ID: 3472854
TEHRAN (IQNA) -Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema ‘kubinya shingo kwa kutumia goti’ ni sera ya daima ya Marekani na kuongeza kuwa: “Katika kipindi chote cha historia, Marekani imekuwa ikitumia sera hiyo kukandamiza madhulumu.

Akizingumza katika kikao cha baraza la mawaziri leo mjini Tehran, Rais Ropuhani amesema Marekani inatumia sera hiyo kuwaangamiza waliodhulumia na kuongeza kuwa Markeani inataka kujifanya kuwa polisi ya dunia.

Itakumbukwa kuwa, mnamo Mei 25, afisa wa polisi katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesta nchini Marekani alimbinya shingo kwa kutumia goti kwa dakika 9 hivi George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika hadi akakata roho.

Muaji hayo ya kikatili chini ya kaulimbiu ya "Siwezi kupumua" matamshi yaliyosikika yakitoka kinyonge kinywani mwa Floyd alipokuwa akiuawa, yanaendelea kushuhudiwa ndani na nje ya Marekani.

Rais Rouhani pia ameashiria kufutwa vikwazo vyote vya silaha dhidi ya Iran baadaye mwezi Oktoba mwaka huu na kusema Marekani imeghadhabishwa na mpango wa kufutwa vikwazo hivyo na sasa inapanga njama ya kutaka vikwazo hivyo visalie.

Amesistiza kuhusu ulazima wa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusimama kidete mbele ya njama hiyo ya Marekani.

Rais Rouhani amesema Iran inatarajia kuwa wanachama wa Baraza la Usalama watasimama kidete mbele ya njama za Marekani kwa ajili ya uthabiti wa kimataifa ambao ulikusudiwa katika mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA.

Rais Rouhani ameashiria kufeli njama za Marekani dhidi ya Iran na kusema: Wamarekani wafahamu kuwa, iwapo wanalenga kukiuka azimio 2231 na kisha watayarishe azimio jipya dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kujilinda katika hali yoyote ile.

Amekumbusha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliweza kuunda mfumo bora zaidi wa kujihami angani wakati ikiwa inakabiliwa na vikwazo na ikafanikiwa kutungua drone vamizi ya Marekani.

3904133/

captcha